Ali Kiba Apiga Shoo Ya Kifalme Oman
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba ambaye Wiki iliyopita alipiga bonge la shoo nchini Oman amedaiwa kufanya bonge la shoo aambalo limetajwa kuwa la kifalme.
Gazeti la Ijumaa wikienda linaripoti kuwa Ali Kiba aliwasili nchini humo katikati ya wiki iliyopita ambapo alipumzika kwenye hoteli ya nyota tano kabla ya kukinukisha katika ukumbi wa hoteli hiyo aliyofikia ijulikanayo kwa jina la InterContinental, Muscat wikiendi iliyopita.
Ijumaa Wikienda lilizungumza na mmoja wa mameneja wa msanii huyo aitwaye Aidan Seif ambapo alipoulizwa kuhusu mafanikio ya shoo hiyo, alisema anamshukuru Mungu imefanikiwa na kwamba ni muendelezo wa Kampuni ya Rockstar4000 kumuandalia Kiba pamoja wasanii wengine wa lebo hiyo shoo kubwa nje ya nchi.
Unajua bila Watanzania, Kiba muziki wake usingependwa nje kama hivi tunavyopokea mialiko kila kukicha, tunaomba waendelee kutusapoti. Kiba amefanya vizuri sana Oman, watu wameruka mwanzo mwisho hivyo nina amini picha kama hii itatokea maeneo mbalimbali“.
https://www.instagram.com/p/BtqS7UXBgm_/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=hkewas2vl692