Video ya Kajala na Mwanae Yazua Gumzo
Kuna video imekuwa ikismbaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha msanii kajala akiwa na mtoto wake wa kike paula wakiwa wanakatika na video hiyo kusambaaa sana katika mitandao ya kijamii na kufanya mahsabiki kuongea sana.
Hata hivyo baada ya wawili hao kusambaza video hiyo, mashabiki walikuwa na maneno mengi ya kusema huku wakisema kuwa kuna baadhi ya mambo yanayohusiana na maadili ya watoto watakuwa wakiharibiwa sana na wazazi wao kutokana na malezi.
Video hii pia inawarudisha nyuma mashabiki wao na kuanza kusema kuwa inawezekana pia kuwa hata kufeli kwa mtoto huyo kumekuwa kukichangiwa sana na malezi ya mama huyo kwa mtoto wake.
kajala aliwahi kufunguka na kusema kuwa aliumia sana baada ya mashabiki kumuandamana mtoto wake huyo kutokana na ukweli kuwa amefeli lakini hawakupaswa kumsema vibaya katika mitandao, lakini kwa swala hilo la kusambaza video hiyo watu wanaona kuwa swala hilo ni sawa tu.
https://www.instagram.com/p/Btvz1UxBlEp/