“Sitaki Mtoto Wangu Aingie Kwenye Sanaa”-Yusuph Mlela
Muigizaji wa Bongo movie Yusuph Mlela amefunguka na kusema kuweka wazi kuwa hajafikiria kuhusu kumpeleka Mtoto Wake wa miaka Sita aanzae kuigiza.
Yusuph Mlela ana Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka sita aliyezaa na Mpenzi Wake wa zamani Lakini Baada ya kuachana amemuacha na Mtoto na yeye ndio anamlea.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti Risasi Mchanganyiko, Mlela ameweka wazi kuwa hana mpango wa kumuingiza Mtoto wake kwenye Sanaa Mpaka pale atakapokuwa mkubwa na kuamua mwenyewe.
Hapana, sitaki mtoto wangu nimuingize kwenye uigizaji, nataka yeye mwenyewe kama atapenda ndiyo baadaye aingie, lakini sitaki nimtengeneze katika mazingira haya, nataka yeye mwenyewe ndiye achague maisha yake. Pia kama atapenda sanaa, nitamruhusu“.