Barakah The Prince Adai Bado Yuko Juu Kimuziki
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince ameibuka na kudai kuwa hajashuka kimuziki kama ambavyo imekuwa ikidaiwa kwenye Mitandao ya kijamii.
Barakah alikuwa amesiniwa chini ya staa wa Bongo fleva Ali Kiba Kupitia Label yake ya Rockstar 4000 lakini Barakah alijitoa kutokana na kutofautiana na uongozi Wake.
Baada ya kuachana na Label hiyo Barakah amekuwa hana hit song kama zamani na pia amedaiwa kuwa amefulia kimuziki pia kumaanisha hajapata wimbo uliosumbua redioni kwa miaka kadhaa sana.
Katika mahojiano aliyofanya na kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Barakah amekataa Tetesi Za yeye Kufulia na kusema kuwa hakufulia bali aliamua kupumzika na kuwapa nafasi wasanii wengine:
Mimi sijashuka kimuziki Lakini nilikaa pembeni ili kuwapisha wasanii wengine wachanga ili waweze kuonekana, na pia sitaki kukibaliana na usemi kuwa nimeshuka bali nimerudi rasmi na hata ukiangalia hapo nyuma ngoma nilizokuwa natoa nilikuwa siendi kwenye media nilikuwa natoa kwenye Mitandao ya kijamii”.