Fahamu Mzee wa Likwidi Alivyorejesha Furaha ya Ommy Dimpoz
Mwanamuziki Ommy Dimpoz amefunguka na kusema kuwa kipindi chote ambacho alikuwa akumwa na yuko hospitali alikuwa akifarijika sana kila alipokuwa akimwangalia msanii mzee wa likwidi kwa vituko vyake.
Ommy anasema kuwa mara nyingi alikuwa akicheka sana mpaka baadhi ya watu walikuwa wakismhangaa hasa madaktari wake kutokana na furaha aliyokuwa akiipata akimuona msanii huyo jinsa anavyofanya vituko.
Anasema “Yuko jamaa anaitwa piere likwidi, yaani kila nilipokuwa namtazama nilikuwa nacheka sana, hasa ile style yake ya kuongea…haiiiiii…mamaaa…. nakufaaa…mpaka madaktari kule ujerumainwalikuwa wakiniuliza nawajibu tu nkuwa haya ni mambo ya tanzania hamuwezi kuyajua.