Ugonjwa Wangu ni Zaidi ya Ule wa Tekno ;-_Ommy
Msanii Ommy Dimpoz amefunguka alipokuwa akiongea na Millard Ayo na kusema kuwa ugonjwa aliokuwa akiumwa yeye ni tofauti na ule wa Tekno kwa sababu pamoja na kwamba msani mwenzake huyo aliambiwa kuwa alikuwa na matatizo katika koo lakini hakufikia hatua ya kufanyiwa upasuajika kama yeye alivyokuwa amefikia.
Ommy anasema kuwa katika maisha yake alikuwa amezoea kuona na kusikia kuwa watu wanaingia ICU nakutoka na wengine walikuwa wanakufa endapo wanaingia huku, hata alipokuwa akiona katika TV alikuwa hanaona ICU na kuiogopa sana kutokana na sifa zake lakini kitu cha kushangaza tangu aliapoanza kuumwa mpaka sasa anmejikuta ICU ameshaizoea.
Tatizo langu lilikuwa kubwa zaidi, sijui kama tekno alifikia huko kwenye maoperation kama mimi, nilikuwa naziona kwenye tv tu hizo Icu , nilikuwa naambiwa tu kuwa kuna ICU , Nikiambiwa mtu kaingia ICU nilikuwa naogopa na kuona kama kuna taarifa nyingine mbaya inaweza kuja lakini kwa sasa mpaka nimeshazizoea.