Mh.Makonda Akerwa na Tabia ya Watu Kuzushiana Vifo.
Mkuu wa Mkoa wa jijini Dar amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa na tabia ya kusema mambo ya uongo hasa maswala ya kuzushiana vifo kitu ambacho kinakuwa kinaleta kukatisha tamaa hasa kama mtu ni mgonjwa.
Makonda anasema kuwa msanii Ommy dimpoz amekuwa akiugua kwa muda mrefu sana mpaka sasa amerudi kuwa mwenye afya lakini watu wengine wamekuwa wakitangaza kuwa msanii huyo amefariki Dunia.
Mh makonda anasema kuwa watu hao hao waliokuwa wakitangaza kuwa msanii huyo amekufa sasa hivi wako kimya baada ya kugundua kuwa msanii huyo kwa sasa tuo vizuri na anaimba wimbo wa kumsifa bwana.
Mh Makonda anasema kuwa endapo ingetokea kweli msanii huyo angepoteza uhai wake basi kila mtu angeweka katikamtandao RIP na kuanza kulalamika kuwa msanii huyo ameondoka bado wanamuhitaji.