Wema kuonekana kwenye CopsEnenmy
Mwanadada Wema Sepetu pamoja na kwamba wengi wanajua kuwa alikuwa katika adhabu ya muda mrefu kutokana na kufungiwa kutokufanya kazi yoyote ya sanaa, anaweza kurudi tena hewani na kuonekana katika video mpya ya CopsEnemy ambayo pia kuna mkono wa zamaradi mketema.
Mwanadada Wema ambae kwa sasa amekuwa akitumikia kifungo chake kutoa chama cha wasanii wa filamu, anaweza kuonekana tena kwa sababu movie hiyo iliweza kuchezwa nae kabla hajapata adhabu hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuinadi muvi hiyo, meneja wa Wema Sepetu neema ndepanya anasema kuwa filamu hiyo inategemea kutoka hivi karibuni na wema atakuwepo kwa sababu haliweza kucheza kabla ya kupata adhabu.
Anasema kuwa , wema amekuwa akifata masharti yote ya adhabu na adhabu hiyo ambayo imekuwa imekuwa ya awamu tatu na wameshamaliza awamu mbili hivyo wanasubiri kumalizia kwa sasa.