Dr. Cheni Baba Yangu Wa Sanaa- Lulu
Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amefunguka na kuongelea uhusiano wake na muigizaji mkongwe wa Bongo movie Dr. Cheni.
Kwa miaka mingi sasa Lulu ameonekana kuwa karibu sana na Dr. Cheni na sasa anafunguka na kuweka wazi kuwa ni mtu wa muhimu kwenye maisha yake.
Katika mahojiano aliyofanya na Kituo cha Times Fm, Lulu amefunguka na kusema kuwa watu wengi hawajui uhusiano Wake na Dr. Cheni Lakini yeye amemtaja kama baba yake katika Sanaa.
Watu wengi hawajui Lakini Dr. Cheni ni baba yangu wa Sanaa, tangu alipogundua kipaji changu Nikiwa na miaka mitano, amezidi kuwa mtu wa muhimu kwangu katika kuikuza na kuiendeleza Sanaa yangu”.
Lakini pia Dr. Cheni ameonekana na Lulu katika wakati ambao alikuwa anapitia kipindi kigumu ikiwemo wakati ambao aliwahi kupelekwa jela.