Harmonize Asimulia Ugumu wa WCB
Harmonize akiwa mmoja ya wasanii kutoka kundi la WCB anakiri kuwa kumekuwa na ugumu sana kufanya kazi na wasanii wenzake ndani ya wcb kwa sababu katika lebo hiyo kwa sababu kila mmoja amekuwa na uwezo mkubwa sana katika lebo hiyo.
Harmonize ambae kwa sasa ni moja ya wasanii wanaotamba sana duniani anasema kuwa ndani ya WCB kila msanii amekuwa akifanya kazi kwa moyo na nguvu ili kutoa wimbo wa kumzidi mwenzake kitu ambacho kinakuwa kinaleta utata sana katika kufanya wao wapate ugumu sana.
Harmonize anasema kuwa ugumu unakuja kwa sababu kila msanii anataka kufanya kazi ili ku-win mashabiki na soko la muziki , hivyo kama unataka kufanya inabidi ufanye kwa bidii kwa sababu hakuna msanii atataka kulegea .