Ommy Dimpoz Afunguka Baada Ya Kurejea Nchini
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amerejea nchini Tanzania rasmi kutoka majuu alipokuwa kwa ajili ya matibabu.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam wakati akirejea nchini Ommy Dimpoz amesema haamini kama amerudi nyumbani licha ya watu mbalimbali kumzushia kuwa amekufa.
Hali kama unavyoiona mimi mwenyewe siamini naona nimefika nyumbani, kiukweli kuhusu uzushi wa kifo nishazoea kwa sababu ya kazi niliyoichagua inatufanya tuzoee hali kama hii. Lakini wanachojisahau duniani wote tunapita kila mtu atakufa na mimi nitakufa, kuhusu kuanza kuimba kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote“.
Ommy Dimpoz alianza kuumwa mwaka jana Baada ya kuwekewa sumu na kusababisha kulazwa nchini Africa ya Kusini kwa miezi kadhaa ambapo alifanikiwa kutoka na kupona kabisa Lakini mwaka jana mwishoni ilisemekana kuwa amezidiwa tena na kutajwa kuwa nchini Ujerumani kwa ajili ya matibabu.