Suzy Asherekea Birthday na Wafanya Usafi Barabarani
Mtangazaji wa kipindi cha Enews cha East Africa Television, Suzan Bernard maarufu kama Suzy amefunguka na kuweka wai sababu iliyomsukuma Mpaka kufagia barabara siku ya birthday yake.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Suzy alisema kuwa mastaa wengi wamekuwa wakisherehekea siku zao za kuzaliwa kwa kuwaangalia watu wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na wagonjwa lakini kwake ameamua kuja kivingine kwa kujichanganya na wanawake wanaohatarisha maisha yao katika kufanya kazi ya usafi barabarani.
Nikiwa kama mwanamke, nawaona wanawake wenzangu wakifanya usafi huu katika wakati mgumu, kuna wengine wanaishia kujifunika na nguo tu puani kwa hiyo kesho (leo) nitahakikisha naingia na mimi barabarani kushiriki nao usafi, baada ya hapo nitawaachia sapraiz ambayo wataiku mbuka maishani mwao“.