“Harmonize Akitua Tu Tanzania Akamatwe Apelekwe Jela”-Makonda
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda amefunguka na kutaka msanii wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize achunguzwe na kama anatumia bangi basi Akamatwe na aswekwe rumande.
Mheshimiwa Paul Makonda ameagiza vyombo vya usalama kumchunguza msanii Harmonize kama anatumia bangi au lah! ili achukuliwe hate za za kisheria.
Makonda amezungumza hayo siku ya jana Alhamisi Januari 31, 2019 wakati akizungumza na wasanii katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam. Amesema katika mtandao wa Instagram ameona picha ikimuonyesha Harmonize anayetamba na wimbo Paranawe akivuta kitu hicho hivyo ameomba ichunguzwe kama ni bangi au lah
Nimemuagiza Gavana wa huko achunguze ile ni bangi au nini na ikigundulika ni bangi atakapotua tu hapa ni pingu na kupelekwa lock up, Vizuri namlea mwenyewe na mtoto anapokosea lazima umshikishe adabu bila kujali unampendaje”.