Idris Azungumzia kukutana na Wema
Msanii Idris Sultan amefunguka na kusema kuwa tangu mwanadada wema sepetu apungue mwili wake na muonekano mpya na hata kufungua duka lake la nguo bado hawajaonana kwa muda mrefu na hata muonekano wake huo mpya amekuwa akiuona kwenye kwenye mitandao tu.
Idris anasema kuwa hawajawahi kukutana lakini amekuwa akimpigia simu na hata kumpongeza kwa sababu ya kufungua duka la nguo za watoto.
Tangu Wema apungue sijawahi kukutana nae lakini nilimpigia simu kumpongeza kuhusu kufungua duka lake, ila tu kwa sasa kila mmoja amkuwa akifanya mambo yake.
Wawili hao waliwahi kuwa katika mahusiano kwa miaka kama miwili iliyopita, lakini kila mara ema anasema pamoja na kwamba wameshaachana lakini hawezi kumchukia Idris.