Wasanii Wengi Wana Majina Makubwa Lakini Pesa Hakuna-Darassa
Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Darassa CMG ambaye amewahi kusumbua sana kwa ngoma yake ya Muziki ameibuka na kuweka wazi hali halisi ya wasanii wengi wa Bongo.
Darassa amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi Bongo wana majina makubwa na hata mashabiki wengi kwenye Mitandao ya kijamii Lakini kiuhalisia hawana pesa na wanaishi katika maisha magumu sana.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Darassa amezungumza mambo mengi sana ambayo ni shule kwenye maisha ya kawaida na Muziki wa Tanzania, lakini anakiri kuwa hakufaidika kwenye nyimbo alizotoa hapo kama jinsi alivyokuwa maarufu.
Kwenye muziki wetu kutengeneza jina ni rahisi sana, lakini kutengeneza fedha ni kazi sana, mimi nilitaka kuwa kwenye daraja ambalo nalitaka lakini kuna ambao wapo wanaotaka kukuonyesha kuwa hicho unachofanya siyo sahihi, njia ya kupita ni huku”.
Baada ya kimya kirefu cha mwaka mzima hatimaye mwaka jana mwishoni Darassa aliachia ngoma yake ya ‘Acha Njia’ ambayo bado inafanya vizuri kwenye vituo mbali mbali vya redio.