Mfahamu Cassie Kabwita , Mwanadada Alietaka Kuchora Tatoo ya jina la Kajala
Mwanadada Cassie Kabitwa kutoka nchini Zambia ni moja ya wasanii waaofanya vizuri katika maigizo nchini humo huku kwa hapa tanzania akiwa ni rafii mkubwa wa masnii Kajala Masanja.Kajala na cassie walishafanya kazi nyingi pamoja na wamekuwa na urafiki mkubwa hata wa kuwa kama mtu na dada yae kutokana na ukaribu wao huo.
Cassie anasema kuwa amekuwa akimpenda sana Kajala kiasi kwamba alitaka kuchora tatoo yenye jina la kajala lakini hakuruhusiwa na Kajala mwenyewe baada ya msanii huyo kumkalisha chini Kajala na kumwambia hasara za kuchora tattoo mwilini.
Cassie anasema , hakuona ajabu kuchora tattoo kuonyesha mapenzi kwa rafiki yake huo ambae kwa sasa amekuwa kama dada, lakini kajala nae hakutaka kuonyesha mapenzi ya kinafiki kwa kutaka kuchorwa tattoo ilhali anajua hasara za tattoo hivyo alikaa nae chini na kumuelezea swala hilo na waliweza kuelewana kabisa.