Hakimu Ataka Kesi ya Wema Iishe
Kesi ya mwanadada Wema sepetu ambayo ilitegemewa kusomwa January 28 inaendelea kuhairishwa tena kutokana na upeplezi kutokamilika kitu ambacho kimekuwa pia kikimkwaza hakimu anaeshughulikia kesi hiyo.
Kesi hiyo iliyopelekwa na mamlaka ya mawasiliano kutokana na kuvujishwa kwa picha na video chafu za mwanadada huyo katika mitandao ya kijamii imekuwa ikipigwa tarehe kila siku.
Hakimu mkazi wa kisutu Maira Kasonde anaeshughulikia kesi hiyo amewaomba wanaochunguza kesi hiyo kufanya uchunguzi haraka na sio kila siku kuwa inapigwa tarehe kutokana na upepelezi.
hata hivyo hakimu wa Wema Sepetu pia analalamika na kusema kuwa kesi hiyo imekuwa ikipelekwa mbele zaidi ya mara nne sasa .
Ikumbukwe kuwa kesi ya Wema Sepetu ilipelekwa mahakama Novembe 2018