Mbosso Aanika Siri Yake Kubwa Ya Udogoni
Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB ambaye pia anayefanya vyema na wimbo wake wa ‘Hodari’ Mbosso ameanika siri yake kwamba alipokuwa mdogo alikuwa anapenda sana kula ubwabwa na maharage kiasi kwamba kuna siku moja ulitaka kumtoa roho kwani alijikuta akivimbiwa kupitiliza.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Mbosso alisema kuwa alipokuwa mdogo alikuwa anapenda sana ubwabwa na maharage kupita maelezo, ukipikwa nyumbani kwao alikuwa hachezi mbali na jikoni, mapema anakuwa amesharudi kwenye michezo yake tayari kusubiria mnuso.
Sijui ilikuwa ni uroho au nini, yaani nilikuwa napenda ubwabwa na maharage kiasi kwamba kuna siku nilivimbiwa sana, ilikuwa kila nikila sishibi, mwisho wa siku ikawa balaa, ikabidi mama achukue mwiko, akanipigapiga nao tumboni, hiyo ndiyo ikawa nafuu yangu, yaani ilikuwa balaa kwani watu walianza kwa kunipepea ikashindikana lakini nilipata ahueni baada ya mama kunipa tiba hiyo”.