Mboso Atangaza Ndoto Yake ya Kumnunulia Diamond Nyumba ya Kifahari
Msanii kutoka kundi la WCb mbosso amefunguka na kusema kutokana na mafanikio yake anayoyapata kutoka WCB anaona kuwa hana kitu cha kumlipa bosi wake diamond platinumz kwa sasa anaona aliyofanyiwa ni makubwa kuliko anachoweza kukitoa yeye.
Mbosso anasema kuwa , amekuwa akiwaza kila siku kitu cha kumpa lakini hakioni lakini ndoto yake kubwa ni kumnunua bosi wake nyumba kubwa au gari la kifahari kama zawadi ambayo pia anajua haitatosha kuonyesha shukrini zake zaidi ya sala .
Mbosso anasema kuwa kila mmoja yuko na njia yake ya kusema shukrani, kama harmonize aliamua kuchora tatoo isiyofutika kama shukrani ya uwepo wake na umuhimu katika maisha yake lakini yeye anaona bado kuna kitu kikubwa anaweza kufanya ingawa kwa sasa amekuwa akimuombea kila kukicha.