Tanasha Ana Kila Sifa Ya Kuwa Mke Wangu- Diamond Platnumz
Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefunguka na kumwagia sifa kibao Mpenzi wake ambaye ni mrembo kutoka Mombasa Kenya Tanasha Donna Oketh.
Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao wa Dizzim Online Diamond amemwagia sifa mke Wake mtarajiwa na kusema mbali na mambo mengine Lakini mrembo huyo anajua sana kupika.
Ni mwanamke pekee aliyenionesha yupo makini na ana sifa zote za kuingia naye kwenye ndoa na sasa ni rasmi ninatangaza kwamba ninamuoa…
Ana sifa zote ambazo mwanaume yeyote aliyekamilika angetamani awe mkewe. Sisi wanaume tulio wengi huwa tunaangalia shepu, maumbile, mvuto wa nje na mengineyo ambayo yote anayo. Lakini kikubwa zaidi kuliko vyote ni TABIA! Ana tabia nzuri”.
Diamond alitangaza kufunga ndoa na Tanasha muda mfupi tu Baada ya Kukutana ambapo mara ya kwanza ndoa ilitakiwa ifungwe mwezi wa pili katika siku ya wapendanao Lakini imesogezwa mbele.