Kajala Akiri Kuchukizwa na Ubonge Wake
Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja amefunguka na kuweka wazi kuwa anachukizwa sana na mwili wake ulivyokuwa kwa sasa Baada ya kunenepa sana.
Kajala ameweka wazi kuwa kati ya vitu ambavyo anavichukia kwa sasa ni pamoja na mwili wake kuwa mnene kupitiliza.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Kajala amesema kuwa ubonge wake kwa sasa umefikia kiasi cha kumnyima raha kwani hata nguo zake nyingi ameshi-ndwa kuzivaa kwa sababu hazimpiti mwilini.
Jamani huu mwili mpaka nahofia naweza kupata presha au gonjwa lolote linalotokana na kunenepa sana maana hata mazoezi naona sasa yamedunda, najitahidi kupambana ili niweze kurudi kama zamani”.
Kajala ametangaza kuongezeka mwili kutokana na maisha ya stare he anayoishi kwa Hivi sasa hasa kutokana na mkataba Wake na Biko ambao unamuingizia mkwanja mrefu.