Q-Boy Ajutia Kuwakosea WCB
Msanii aliyewahi kufanya kazi ndani ya Wcb Q-Boy amefunguka na kusema nkuwa katika maisha yake bado aanajutia sana kuwakosea wcb mpaka kushindwa kuendelea kufanya nao kazi kama hapo awali.
Msanii huyo ambae aliondoka wcb lakini hakusema moja kwa moja ni kitungsani kilimfanya aondoke wcb anaonekana kujutia kosa alilolifanya wcb mpaka kuacha kufanya kazi na lebo hiyo.
q-Boy anasema kuwa hata kama angekuwa na pesa nyingi kaisi gani bado asingeacha kwenda kwaomba msamha alebo hiyo ili waweze kumsamehe ,hii ina maana kuwa kufanya kazi na lebo hiyo kuna thamani kubwa sana kwake kuliko hata pesa anazoweza kuwa nazo.
Hata kama ningekuwa na pesa kama bakhresa bado ningerudi wcb kuomba msamaha.
Ikumbukwe kuwa wcb ni moja ya lebo kubwa nchini na inawezekana kuwa ndio ya kipekee kwa sasa inayofanya vizuri na wasanii wake na ndio lebo kubwa ambayo kila msanii amekuwa na ndoto ya kuifanyia kazi.