Esma Apiga Dua Ndoa Ifanikiwe
Mwanadada esma platinumz ambae ni dada wa msanii Diamond platinumz amefunguka na kuonyesha wasiwasi wake katika swala zima la kufungwa kwa ndoa kati ya kaka yake na mwanadada tanasha kutoka nchini kenya.
Esma ameonekana kuwa na wasiwasi huo mpaka kufikia hatua ya kushusha sala katika moja ya picha aliweka kaka yake kuhusu mwanamke wake huku akiomba ndoa iyo itimie.
Ukiachana na walimwengu kuwa na wasiwasi na kusema ndoa hiyo haiwezinkufanikiwa, hayo yote yanakuja kutokana na kutokuwa makini kwa Diamond platinumz amvae anakuwa na mahusiano na wamawake tofauti na kutangaza ndoa lakini kushindwa kuwaoa.