“Nisingehangaika na Muziki Ningekuwa Najiuza”- Lulu Diva
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka na kuweka wazi kuwa muziki umemsaidia kutoingia katika ulimwengu wa madada poa.
Lulu Diva ameushukuru muziki na kusema kuwa kama asingefanya juhudi binafsi katika muziki wake angekuwa miongoni mwa wanawake wenye mwonekana hasi kwa jamii.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba, Lulu Diva amesema kuwa awali alikuwa na ndoto za kuamini uzuri wake umetosha kumfanya aishi mjini, kitu ambacho kilikuwa mawazo potofu, kwani anaamini kama angeendelea hivyo asingeweza kufikia ndoto zake.
Ukweli nilizungukwa na marafiki ambao hawakuwa na ushauri mzuri kwangu, nilikuwa naamini uzuri wangu ndio kila kitu, kama nisingekaza kwenye muziki basi ningekuwa mmoja wa wanawake wanaojiuza mjini”.
Hivi sasa Lulu Diva anafanya vizuri katika tasnia ya Bongo fleva na pia amepata mafanikio makubwa ikiwemo kununua Nyumba na gari zuri.