Hakukuwa na Ndoa Kati ya Irene na Dogo Janja, Kilikuwa Kivuli :-Mwijaku
Mwigizaji msemaji sana Mwijaku amefunguka na kuongelea swala la ndoa ya Irene na ndogo janja kuvunjika na kusema kuwa tangu hapo awali aliwahi kusema swala hilo kuwa hakuna ndoa kati ya Irene na dogo janja kwa sababu irene hakuwa na aiba ya kuwa mke wa mtu.
Akisiistiza maneno yake , mwijaku anasema kuwa kati ya wawili hao waliofunga ndoa mwaka uliopita na ndoa hiyo kuvunjika mwaka huo huo , hakukuwa na ndoa kati yao zaidi ya kuwa walikuwa wakitaka kutengeneza matukio tu.
Ikumbukwe kuwa wawili hao walifunga ndoa ambayo ili-trend sana katika mitandao na kila mmoja alikuwa akiwaongelea kila wakati lakini ghafla wawili hao waliishia njiani na ndoa kuvunjika huku sababu kubwa ikiwa ni swala la michepuko.
Mwijaku anasema swala kubwa lilikuwepo ni kuwa dogo janja alikuwa akiongozwa na Irene na ndio maana ndoa imeshindwa kudumu , lakini kule alipo sasa hivi wanaweza kudumu kwa sababu wanaonekana wapo katika level zinazofanana na kwamba inaonekana kuwa kule amempenda mwanamke kwa kufuata moyo wake.