Msanii Tekno Adaiwa Kumuiga Diamond Kwa Hili
Msanii wa muziki kutoka Nchini Nigeria anayefanya vizuri kabisa maarufu kama Tekno Miles amedaiwa kufuata nyendo Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa kufungua Music Label yake.
Tekno ameingia Kwenye Listi ya wasanii wengi wa Afrika ambao wanafanya vyema kama vile Wizkid, Davido, Patoranking kwa kumiliki Music Label yake inayokwenda kwa jina la Cartel Music.
Meneja wa msanii huyo, ‘John Peace’ amethibitisha taarifa hizo katika mtandao wa burudani nchini Nigeria kwamba Tekno ameondoka katika lebo yake ya awali ya Triple MG na kuelekea kwenye lebo yake aliyofungua ya Cartel Records.
Msanii huyo pia amejitambulisha kuwa yeye ni mmiliki kamili wa lebo hiyo kwenye akaunti yake ya instagram kwa kuweka picha yenye jina la lebo yake ikiwa na maelezo yanayosomeka ‘CEO’.