Rammy Galis Alamba Shavu Nono Katika Tuzo za ZSIFF
Muigizaji wa Bongo movie Rammy Galis amejikuta akiwa na Shavu Nono Kupitia tuzo maarufu katika tasnia ya Bongo movie tuzo za Zsiff.
TAMASHA la Tuzo za Sinema Nchini lijulikanalo kama Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) limezinduliwa rasmi usiku wa kuamkia jana Jijini Dar es salaam.
Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Sinema ulipo jengo la City Mall katikati ya jiji la Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Balozi wa Kenya hapa nchini, Dan Kazungu.
Katika uzinduzi huo, baadhi ya wageni waalikwa walipata nafasi ya kuangalia sinema ya kutoka hapa nchini iitwayo Red Flag ambayo imeigizwa na Mtanzania, Rammy Galis.
Sinema hiyo ndiyo pekee ya kutoka Tanzania ambayo itashindanishwa na nyingine 31 kutoka mataifa mbalimbali.
Rammy Galis amepata shavu hilo kutokana na sinema yake hiyo kudaiwa kukidhi viwango vya kimataifa kutokana na kutumia Lugha ya Kiingereza.