Mch.Mashimo Amcharukia Mama Amber Ruty
Mama wa msanii Amber rutty aliwahi kusema katika mitandao ya kijamii kuhusu swala la mchungaji mashimo kumtolea dhamana mwanadada Amber Ruty na kusema kuwa yeye ndio aliyekuwa mdhamini wa mwanae na wala sio mtu mwingine kama ambayo inasemwa katika mitandao ya kijamii.
Lakini mchungaji mashimo amefunguka na kuonyesha kukerwa na tabia hiyo na kusema kuwa yeye ndio aliyehusika na dhamana ya msanii huyo huku wakati mwingine hata akituma pesa ya matumizi kwa ajili ya walengwa hao ingawa anahisi kabisa kuwa pesa hizo hazikuwa zikiwafikia walengwa.
Mchungaji huyo aliwahi kusema kuwa kufabya kwake hivyo hakumaanishi kuwafungwa sanii hao kuchana na imani yao lakini yeye alifanya kwa sababu alikuwa akiongozwa na mungu kufanya hivyo.