Faiza Ally Akiri Kuwahi Kuwa Mdangaji
Mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, Faiza Ameibuka na kuweka wazi kuwa ameshawahi kudanga.
Faiza Ally ameeleza kuwa kudanga kwake siyo ishu kwani kama mtu anafanya hivyo kwa kufanya kitu cha maana siyo tatizo Kama atatumia kama njia ya kufanya mambo ya maana.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Faiza alisema kama ni kudanga amedanga, lakini alifanya hivyo kwa malengo fulani kwa sababu hakuna anayependa kudanga, alipotatua shida yake kwa sasa amekuwa shujaa na anayejitokeza na kumcheka hajitambui.
Nilidanga kwa sababu zangu nilizokuwa nazo na mwisho wa siku naendelea na maisha yangu”.
Faiza amefungukia biashara zake anazomiliki kwa Hivi sasa ikiwemo tenda ya kuagizia wateja bidhaa kutoka nchini China kuja Tanzania.