Aikah Afunguka Kukosa Raha Kisa Ubonge
Msanii wa Bongo fleva kutoka katika Kundi la Navy Kenzo Aikah Marealle amefunguka na kuweka wazi Jinsi miwili mkubwa unavyokuwa unamnyima raha hasa stejini.
Aikah ambaye ameonekana kukosolewa sana na mashabiki zake hasa katika Mitandao ya kijamii amefunguka na kukiri kuwa anajua kabisa ameongezeka sana lakini anafanya jitihada za kupungua.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Aika alisema amekuwa akiteseka na ubonge alionao kwa sasa kwani haupendi na watu mbalimbali wamekuwa wakimshangaa na kumtaka aanze kufanya mazoezi kwani anapoteza mvuto.
Siupendi ubonge nilionao kwa sasa, mashabiki wangu kibao wamenitaka nianze kufanya mazoezi kwa sababu kunenepeana huku napoteza mvuto. Nimepokea maoni yao na nitaya fanyia kazi maana nimejikuta nanenepa kutokana na uzazi”.
Aikah ambaye ana Mtoto wa mwaka mmoja na Mpenzi Wake Nahreel ameweka wazi kuwa alizidi kuongezekabzaidi Baada ya kujifungua mwaka jana.