Esma Asema Hamisa Anaharibiwa na Watu
Dada wa msanii diamond platinumz amefunguka na kusema kuwa moja kati ya vitu anavyojua kuhusu Hamisa Mobeto ambae aliwahi kuwa mpenzi wa kaka yakena hata kupata bahati ya kupata mtoto mmoja ni kwamba mwanadada huyo aana tabia nzuri sana lakini amekuwa akiharibiwa na watu.
Akijibu maoni na maswali ya mashabiki zake katika ukurasa wake, Esma anajibu swala liloulizwa na shabiki maoni yake juu ya Hamisa na ndipo anasema hivyo.
Ikumbukwe kuwa mwanadada hamisa na sma walikuwa marafiki wakubwa sana kipindi cha nyuma , lakini ghafla hamisa na familia yote na diamond walikuja na kuwa maadui na hata kufikia hatua ya kuitana wachawi mbele ya mashabiki mitandaoni.