Rosa Ree Adai Bado Mdogo Mambo Ya Mapenzi Hataki
Msanii wa Bongo fleva anayefanya hip hop pia Rose Robert maarufu kama Rosa Ree ameibuka na kudai kuwa sababu inayomfanya asiharakishe kuingia kwenye mapenzi ni uamuzi.
Rosa Ree ameibuka na kudai kuwa anapokuwa hayupo kwenye mapenzi haimaanishi kuwa hakuna watu wanaomfuta kwa lengo la kumshawishi Lakini yeye mwenyewe ameamua kutulia kwenye sekta hiyo.
Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Rosa Ree amesema kuwa anaamini kuwa umri wake bado mdogo hivyo hana papara na mapenzi.
Mapenzi yapo, napenda familia yangu, nampenda Mwenyenzi Mungu, napenda pesa, mimi mdogo sana, am very young, yaani sio kwamba hawapo ambao hawatamani kuwa na Rosa Ree lakini hatuendani”.
Ingawa Rosa Ree ameshatajwa kuwahi kuwa kwneye mahusiano na wasanii Kama Young Dee na Bill Nas Lakini aliwahi kukataa na kusema kuwa wale ni washkaji zake tu.