Kim Nana Amwaga Povu Kisa Penzi la Diamond na Tanasha
Video vixen na mwanamitindo Lilian Kessy maarufu kama Kim Nana amejikuta akimwaga Povu zito Baada ya kuulizwa kuhusu Ex Wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Mpenzi Wake Mpya Tanasha Donna Oketh.
Kim Nana alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Diamond kwa muda kabla ya kumwagwa chini miezi michache iliyopita na Diamond kuanza mahusiano na Tanasha.
Kim Nana ameibuka na kulitolea povu penzi jipya la Diamond na Tanasha baada ya Gazeti la Amani kumtaka azungumzie penzi jipya la Diamond ambaye awali iliaminika kuwa ndiye mumewe mtarajiwa kabla jamaa huyo hajaibuka na Tanasha.
Akimzungumzia zilipendwa wake huyo, Kim alisema mambo ya Diamond na Tanasha hayamhusu huku akielekeza lawama zote kwa mitandao ya kijamii.
Hivi mnajua kiasi gani nimetukanwa kwenye mitandao ya kijamii? Na pia watu wa mitandao hawajui kabisa kufuatilia vitu kwa kina wanachojua ni kutukana watu lakini nashangazwa sana mimi kuhusishwa na Diamond, naomba kuweka wazi leo siko kwenye mapenzi na Diamond kwa sasa mimi nina maisha yangu na yeye hivyohivyo ndiyo maana amemuweka wazi mpenzi wake mpya kama ningekuwa ni mimi si angewaambia mashabiki zake kuwa ni mimi?”.