Nisha Bebe Akana Tuhuma Za Kumiliki Kibenteni Kipya
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nisha Rajabu ameibuka na kutolea povu Tetesi za kutoka kimapenzi na kijana ambaye amemzidi umri (Kibenteni).
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Nisha Bebe amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa kwa sasa yupo mapenzini na mtu ambaye asingetamani kumuweka wazi na amemzidi umri na kwa upande wa Watanzania ameshamalizana nao.
Kuna kitu wacha nikiweke sawa, kuna post niliona kama sio jana basi juzi inasambaa kunihusu sijui nna kiben ten mpya sijui nini na nini.Wapendwa huko me nimeshavuka tangu 2016,nilishaapa kutokudate na mtu niliyemzidi umri pamoja na kipato,na kudate Mtanzania mwenzangu kwangu ni mwiko tena”.
Wakatimwingine tunakaa kimya kutokana na kuona kujibu jibu ni utoto,niko kwenye miaka ambayo hatudhungumzi sana,hatuna show off,tunaishi maisha yetu na tunapunguza mambo mengi ambayo siyo ya msingi”.
https://www.instagram.com/p/BsS2bNLA13A/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1g3lrkoj7s6py