Kigogo Anayesimamia Bata Za Uwoya Aanikwa
Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amedaiwa kuishi maisha ya bata ndefu kwa sababu ya Kigogo mwenye pesa zake ambaye ndio mpenzi wa Uwoya kwa sasa.
Gazeti la ijumaa Wikienda linaripoti kuwa mtu wa karibu na Uwoya amepasua kuwa Uwoya anapewa jeuri ya pesa na kigogo mzito aliyepo kwenye Serikali ya Kenya.
Ni kigogo (anamtaja jina, tunalihifadhi sababu hatujampata kuthibitisha) katika Serikali ya Kenya, ndiye ambaye anamuwezesha kwa kila kitu. Hizi sijui kufuru za bethidei yake, sijui kujiachia kwenye boti hadi Zanzibar kigogo huyo ndiye anayemuwezesha”.
Chanzo hicho makini kilizidi kwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa, kutokana na uzito wa kigogo huyo, imekuwa ngumu kujulikana na hata anayejua pia huhofia kusema.
Ni kutokana tu na uzito wa kigogo huyo na bahati mbaya sana ni kwa sababu yupo Kenya, ingekuwa yupo Bongo ingekuwa ni rahisi sana watu kumjua.
Kigogo huyo ndiye anayedhamini pia zile safari za mara kwa mara za Uwoya nchini Dubai, nafikiri huwa wanakutania huko na huyo kigogo kula zao raha.”
Baada ya tetesi hizo Gazeti hilo lilimsaka Uwoya ambaye alifunguka na kuweka wazi:
Hivi kwa nini kila mtu anapenda kumjua mtu wangu maana marafiki wanapenda kumjua, wasanii wenzangu, mpaka ndugu zangu yaani watu wanahangaika kweli jamani Lakini Huyo (anamtaja jina) nampenda sana labda niseme hivyo, siku akija Bongo watu watafunga midomo yao”.
Uwoya alisisitiza kuwa hawezi kumtaka Mpenzi Wake kwa sasa Lakini muda ukifika atamuweka wazi.