Queen Darleen Aanika Tabia Yake Mbaya
Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika Kundi la WCB, Mwanahawa Abdul maaruufu kama Queen Darleen amefunguka na kuanika tabia yake mbaya.
First Lady wa WCB amefunguka na kuweka wazi kuwa, alipokuwa mdogo alikuwa chauroho kwani alipenda sana kukomba chakula akiwa anakula na watu wengi.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Queen Darleen alisema alifikia hatua ya kuonekana na tabia hiyo kwani kila alipokuwa anakula kwenye sahani au sinia na wenzake, alikuwa akikomba chakula na kujikusanyia upande wake.
Nilikuwa na tabia mbaya sana, yaani tukiwa tunakula wengi kwenye sinia halafu nione kama wananizidi spidi, naanza kukomba chakula, najikusanyia upande wangu yaani nilikuwa mroho kupitiliza, ila mama yangu aliikomesha hiyo tabia kwa sababu ilikuwa ikitia aibu mbele za watu”.
Queen Darleen alifunguka maisha hayo aliyokulia uswahilini ‘Tandale’ pamoja na kaka yake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.