Madee Ali – Ni Ruksa Mwanangu Kufananishwa na Mai
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Madee Ali amedai ni ruksa kwa watu kumfananisha mwanaye mdogo anayejulikana Kama ‘Chonge’ na Mtoto muigizaji Mai Zumo.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Madee amesema kuwa hana neno pale anapoona watu wanafananisha Mtoto Wake na Mai Zimo kwani duniani wawili wawili.
Nimekuwa nikiona mara nyingi watu wakimfananisha binti yangu Chonge na huyu mtoto mchekeshaji Mai Zumo, ni kweli wanafanana na huwa sichukii kwa sababu ni jambo la kawaida.
Lakini Pia duniani watu wawiliwawili, hivyo Mungu akitujalia, basi itabidi wafanye kitu cha pamoja ili tutengeneze pesa.”
Mtoto wa Madee, Chonge na Mai Zumo mara kadhaa wamekuwa wakifananishwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na sura zao kufanana.