Napenda Kumpumzisha Mke Wangu- Chiddi Mapenzi
Mfanyabiashara maarufu kwenye Mitandao ya kijamii Chiddi Mapenzi Ambaye pia ni Mume wa staa wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kudai anapenda kumpunzisha mke wake.
Chiddi Mapenzi na mke Wake Shamsa wanamiliki duka la nguo ambalo ndilo linawaingizia kipato na mara nyingi Shamsa amekuwa akionekana kama ndio msimamizi wa duka hilo.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Chiddi ameweka wazi kuwa hapendi kabisa kumchosha mke wake kwa kumuweka dukani kila siku badala yake anapenda kumuona akiwa amepumzika nyumbani.
Ukiona Shamsa yupo dukani ujue kabisa mimi sipo, nimesafari, lakini kama nipo mjini, siwezi kumruhusu kukaa dukani.
Namuonea huruma sana, kuna kipindi anachoka halafu yeye ni mama, ana majukumu mengine anafanya ya nyumbani hivyo anapopumzika ni vizuri”.
Lakini pia Chiddi amezima kabisa tetesi za wawili hao kuachana ambazo zilizuka baada ya Shamsa kuweka kauli tata kwenye social media.