“Mwaka 2018, Nilitimiza Ndoto Zangu”- Vanessa Mdee
Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Vanessa Mdee maarufu kama ‘Vee Money’ amefunguka na kuweka wazi kuwa mwaka 2018 ulikuwa mwaka mzuri sana kwani alitimiza Ndoto zake nyingi.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Showbiz, Vanessa alisema mwaka 2018 alitimiza baadhi ya ndoto zake ikiwemo kuzindua albam yake ya Money Mondays na viatu vyake ya Bora Star by Vanessa Mdee.
Mwaka 2018 ulikuwa poa sana kwangu, namshukuru Mungu nilitimiza baadhi ya ndoto zangu ikiwemo kuzindua albam yangu ya Money Mondays na viatu vyangu vya Bora Star by Vanessa Mdee, naomba Mungu azidi kunifanikishia zaidi na zaidi mwaka 2019“.
Lakini pia Vanessa habanero mpango wa kuishia hapo kwani 2019 ana mipango makubwa zaidi kibiashara kwani hapo baadae anategemea kuja biskuti cha chokoleti zitakazoitwa Vee Choc.
https://www.instagram.com/p/BnGAQ2FByh2/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1dcqd85ipi7mo