Madee Afungukia Furaha Yake Kuwa Mzazi
Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Hamadi Ali ‘Sheneida’ ‘Madee’ amefunguka na kuweka wazi kuwa hakuna kitu kinachompa furaha kama vile kuwa mzazi.
Madee ambaye ni baba wa watoto wawili wa kike amefunguka kuwa endapo watu watamuona kitaa akiwa amembeba binti yake wasije kudhani kasusiwa na mama yake la hasha ila ameamua mwenyewe.
Wakati wanaume wengi wakisifika kwa kukwepa kulea watoto wao Lakini Madee ameibuka na kudai kuwa kwake hiyo wala si ishu, anapenda kinoma kulea Watoto Wake.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Madee ameweka wazi Furaha anayopata kuwa karibu na Watoto Wake na hasa kuwapa malezi ya baba.
Hakuna kitu kinanipa raha kama ninavyomlea mtoto wangu, yaani nikimuona ananipa nguvu nyingi ya kutafuta pesa ili aweze kukua katika maisha bora yeye na dada yake.”
Madee amewashauri wanaume wenzake kuwepo kwenye maisha ya Watoto wao ili kuvunja Imani za kuwa wamama peke yao Ndio Walezi.