JB Aongelea Kushuka kwa Kiwango cha Bongo movie
Muigizaji wa Bongo movie maarufu JB amefunguka kuhusiana na tuhuma za kushuka kwa kiwango cha filamu za Bongo movies. Watu wengi hasa mashabiki wa filamu hizo wamekuwa wakilalamika kuwa ladha ya filamu hizo imepotea na sio kama zamani na hiyo kuwapelekea wao kushindwa au kuacha kununua filamu hizo na kupelekea kukosa soko kwani watu wengi wamehamia kuangalia filamu za kikorea na kifilipino.
Katika mahojiano aliyoyafanya JB amekiri kuwa kweli filamu hizo zimekosa mvuto kwa watazamaji kwani tatizo ni stori kujirudia rudia na bajet finyu ya kutengenezea filamu hizo.
JB alisema;
“Matatizo ambayo yalikuja kuikumba tasnia ya filamu ukiacha usambazaji ni hadithi, sasa kwa hadithi nyingi hazikuwa siyo nzuri wakati wa kutengeneza filamu, vipi tamthiliya ambayo ni kitu kirefu? ndio maana utaona kuna tamthiliya nyingi sana ambazo zinafanywa lakini hazivumi vile kama ilivyokuwa zamani”.
Mashabiki wengi wa filamu hizo wamekuwa wakiwalaumu waigizaji wa filamu hizo kwa kupoteza mwelekeo wa sanaa na kujiingiza katika vitendo a,bavyo vinaua sanaa zao. mfano wasanii wengi wa kike wamekuwa na skendo nyingi sana ambazo zinawafanya wajulikane sana kwa skendo kuliko vipaji vyao hivyo kupelekea kuua sanaa zao.
Mbali na hayo pia Bongo movie ilipata pigo kubwa sana baada ya kufariki marehemu Kanumba ambaye alikuwa na mchango mkubwa sana katika sanaa hii ambapo alikuwa akivuka boda na kuitangaza bongo movie nje ya Tanzania lakini tangia afariki hajatokea msanii wa kuziba pengo lake.
Je unahisi anaweza kutokea msanii wa kuziba pengo la Kanumba na kuipeleka sanaa hii mbele zaidi ili ikapate soko la nje ya nchi? Tafadhali toa maoni yako.