Nandy Afuata Nyayo za Dogo Janja.
Mwanadada Nandy ameamua kufuata nyayo za msanii mwenzake Dogo Janja baada ya kuonyesha mafanikio yake ya kujenga nyumba mpya kwa ajili ya wazazi wake jambo ambalo anashukuru ameweza kulifanikisha kwa mwaka uliopita 2018.
Mwanadada huyo aliamua kuweka nyumba hiyo katika ukurasa wke wa instagram , ikiwa kama moja ya shukrani zake kwa mwaka 2018 kwa mafanikio yake aliyoyapata.
Mwanadada huyo anasema kuwa ameamua kujenga nyumba hiyo kwa ajili ya wazaiz wake ikiwa kama njia ya mafanikio kwa kazi zake.
Nyumba alionyesha Nandy kuwa ni zawadi kwa wazazi wake kwa mwaka 2018