“Siwezi Kumsaliti Ochu” -Witness Kibonge Mwepesi
Msanii wa Bongo Fleva mkongwe,alieanza musiki miaka mingi iliyopita lakini mpaka sasa bado anawika katika nyanja hizo, ambae pia ni Rapper wa kike anaetumia mwili wake vizuri na haujawahi kumshinda katika kazi zake Witness Kibonge Mwepesi amemsifia mpenzi wake na baba mzazi wa mtoto wake lakini msanii mwenzie pia OchuSheggy na kusema kuwa anampenda sana kuliko kitu chochote na hata kaa amsaliti hata siku moja.Katika ukurasa wake wa instagram Witness aliandiaka sifa hizo nyingi kwa baba mzazi wa mtoto wake huyo kuwa ni mwanaume wa tofauti kuliko watu wanavyodhani , anasema kuwa kwa upande wake hawezi kumsaliti mwanaume huyo labda yeye aanze kuzingua.
“Ninampenda huyu mwanaume, tofauti na mnavyodhani, na siwezi kumsaliti na mtu awae yeyote yule , labda azingue yeye kwa mengine ila kwangu mimi siwezi liharibu penzi letu”ameandika Witness
Witness na OchuSheggy wamekuwa katika mahusiano kwa muda wa miakaa zaidi ya mitano sasa na wamebahatika kupata mtoto mmoja , yeye na mumewe na wamekuwa wakisapotiana katika kazi zao za kimuziki na kuna baadhi ya nyimbo wamekuwa wakiimba pamoja mfano wimbo wa Sharifa “penzi letu linaelekea miaka mitano sasa toka tuwe pamoja na lipo kama ndio kwanza tunatongozana “aliongezea Witness
Witness ameelezea pia sababu inka,ayoyawafanya wawili hao waendelee kupendana na kudumu katika mahusiano yao ya kimapenzi “kilichopo hapa ni chemistry inayotengeneza utulivu wa moyo na si chemicals za kuharibu afya na amani ya moyo!”anaongea Witness.
Wawili hawa wamekuwa moja ya wapenzi wa kuigwa kwa sababu wamekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu huku wote wakiwa ni wasanii lakini imekuwa tofauti kwa mahusiano ya wasanii wa kitanzania ambao mahusiano yao hayawezi kukaa kwa muda mrefu bila kuachana . mahusiano ya wawili hao yamedumu kwa muda mrefu na wanaonekana kujiheshimu na kupendana kama anavyodhiirisha witness mwenyewe.
Witness anaejulikana kwa nyimbO zake kama Mzuka, Jirani aliyomshirikisha Snura na Mzee Yusuph, Buku jero na nyingine nyingi anaweza kuwa mfano wa kuigwa kwa wasanii wa kike.