Esma Ashabikia Ndoa Ya Diamond na Tanasha
Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka na kuweka wazi mapenzi yake kwa wifi yake mpya Tanasha na kuweka wazi kuwa kama kaka’ke huyo atachukua uamuzi wa kumuoa kwake yeye anabariki kwa sababu ni chaguo lake.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Esma hadhani kama ni vyema kumchagulia kaka yake huyo mke, bali macho yake ndiyo yanaona wapi ni bora aangukie hapo na atakapopachagua na kumuonesha atampokea tu.
Unajua hata leo Diamond akimtambulisha rasmi Tanasha kuwa anataka kumuoa, mimi kama dada, nitaona ni jambo la heri kwenye familia yetu ambayo kila kukicha tunamuombea apate mke bora”.
Diamond alianzisha mapenzi na binti huyo wa Kikenya Wiki chache zilizopita Lakini wamekwisha tangaza ndoa yao ambayo itafanyika mwezi wa pili mwakani.