Salamu Za Wasanii Kutoka kwa Ney Wa Mitego
Akiwa ni mmoja kati ya wasanii wanaofanya vizuri katika tasnia hii ya muziki, mwanamuziki wa Bongo Fleva Emmanuel Elibariki Ney Wa Mitego “True Boy” ameamua kuwashauri wasanii wenzie wanaokaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa nyimbo huku wakitegemea kuwa watakapotoa watapokelewa vizuri na mashabiki zao.
Ney wa mitego ameyaongea maneno hayo alipokuwa kwenye mahojiano na kituo cha Televisheni Cha Taifa ‘Tbc’ katika kipindi cha Papaso , Ney Wa Mitego anasema kuwa kwa sasa game la muziki limebadilika sana hivyo si vizuri kwa wasnii kukaa kwa muda mrefu bila kutoa wimbo kama walikuwa wamezoa hapo mwanzo.
“huo muda umeisha, this time mtu akirudia hivyo basi tenaa!!yaani tunamsahahu kabisa, game hilo halipo tena”alisema Ney Wa Mitego.
Kwa muda sasa kumekuwa na tabia za mazoea kwa baadhi wasanii wa muziki kukaa kimya kwa muda mrefu sana bila kutoa nyimbo mpya wamekuwa wakisahau kabisa kuwa wanafanya baadhi ya mashabiki wao kuwa na kiu na kuchoka kusubiri kwa muda mrefu, hata hivyo kutoa nyimbo kila baada ya muda pia kunafanya kukua kwa muziki.
Hata hivyo, katika maneno hayo aliyosema Ney wa Mitego hakuonesha kumlenga msanii yoyote ingawa ni kawaida kwa baadhi ya wasanii wakubwa wa muziki kukaa kimya mpaka mashabiki zao wanaanza kurushiania maneno katika mitandao huku wakimuuliza anatoa lini nyimbo mpya. Kama msanii alikiba ni mmoja wa wasanii wenye tabia ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa nyimbo, hivyo kama msanii Ney Wa Mitego ametaka anajaribu kuwahasa wasanii wenye tabia hizo kuacha kwa sababu game la muziki limebadilika watafikiri mashabiki wanawasubiri kumbe ndo wanawapoteza mashabiki.
Ney Wa Mitego ni moja kati ya wasani ambao nyimbo zao zinapendwa na mashabiki kwa sababu uongea ukweli katika mashairi yake bila kuogopa, mara nyingi amejikuta hata akiingia katika majibizano na baadhi ya wasanii wenzie kwa sababu ya kusema ukweli wao. Kwa sasa anatamba na kibao chake kinachokwenda kwa jina la “Makuzi’