Diamond Platnumz na Rayvanny Wafungiwa Kufanya Show Ndani na Nje Ya Nchi
Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Rayvanny kutokea katika Label ya WCB wamefungiwa rasmi kutofanya show ndani na nje ya nchi kwa muda usiojulikana.
Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limetangaza kuwafungia Diamond na Rayvanny Baada wawili hao kukiuka masharti waliyopewa.
Taarifa iliyotolewa leo Desemba 18, 2018 na BASATA, imesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya wasanii hao kuonyesha dharau kwa mamlaka zinazosimamia shughuli za sanaa nchini, kwa kufanya vitendo vinavyokiuka maadili.
Kwa upande mwingine, BASATA wamefuta kibali cha Tamasha la Wasafi Festival linalotarajiwa kufanyika nje ya nchi baada ya kuzunguuka kwenye baadhi ya mikoa hapa Tanzania.
Imeelezwa kuwa wimbo wa Mwanza ndio uliowaingiza matatani, baada ya wasanii hao wikiendi iliyopita kuonekana jukwaani katika Tamasha la Wasafi Festival jijini Mwanza wakitumbuiza wimbo huo.