Jike Shupa Adai Ujauzito Ndio Umemfanya Awe Kimya
Video vixen na muandaaji maarufu wa vibao kata Zena Abdallah maarufu kama Jike Shupa amefungukia ukimya wake na kuweka wazi kinachomfanya awe kimya ni ujauzito alionao.
Jike Shupa amesema amekuwa kimya sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na majukumu ya kubeba ujauzito lakini amesema akishajifungua tu mtoto wake atarudi kama kawaida.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Jike Shupa alisema kuwa, watu hawasikii purupukushani zake ila akishajifungua, kila mtu atajua ameibuka tena mjini.
Najua mjini kumepoa sana kwa sababu mimi kubwa lao sisikiki, lakini ngoja nizae kwanza, nikikaa sawa, wataisoma namba na vimbwanga vyangu kama kawa“.