Ali Kiba Adai Anacheza Moira Coastal Union Lakini Halipwi Kitu
Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa ingawa amesainiwa kuichezea klabu ya Coastal Union ya mkoani Tanga lakini hawamlipi pesa yoyote.
Miezi michache iliyopita klabu hiyo ilitangaza kumsaini msanii huyo ambaye mbali ya kuimba Lakini pia ana kipaji kikubwa cha kucheza mpira wa miguu.
Lakini Baada ya miezi kupita tangu asainiwe na kutoonekana uwanjani Ali Kiba ameweka wazi kuwa yeye halipwi kuchezea klabu hiyo bali anacheza kwa sababu ya mapenzi aliyonayo kwa mchezo huo na timu yake.
Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Ali Kiba amedai Kupitia kuchezea timu hiyo ameweza kukitangaza kinywaji chake cha Mo Faya Lakini pia na kuitangaza timu hiyo.
Mimi silipwi, sichezei kwa pesa, nacheza for fun napenda kucheza mpira. Vile vile nimeweza kuitangaza Coastal, nimeitangaza Mofaya zaidi. Vile vile Coastal wanaitangaza Mofaya hiyo nayo imenipa Milage sana kwangu mimi”.
Lakini pia Ali Kiba amesema yupo mbioni kuanza kuuza jezi za Coastal Union zenye namba yake (7) na zitakuwa na saini yake na kukiingiza kinywaji cha Mo Faya Sokoni.