Sio Kitu Rahisi Kuwa na Mimi :-Posh
Mwanadad anaejulikana sana katika Mitandao ya kijamii hasa kutokana nakuwa na shepu kubwa Jacquline Obedi amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba amekuwa na umbo la kuvutia kwa kila mwanaume lakini hiyo haimaanishi kuwa inaweza kuwa rahisi kupatwa na mwanaume yoyote .
Posh anasema kuwa yeye hana zile tabia za wadada wa mjini za kudanga na mara zote amekuwa akijihudumia yeye mwenyewe hivyo wala hawezi kujirahisisha kama watu wanavyomuona.
sio kitu rahisi kuwa na mimi ilo unayakiwa ujue, sio mtu ambae ninaweza kuchukuwa vitu vyako kirahisi tu ukahisi hivyo tu ila kama mwanaume wangu anatakiwa kuwajibika tu na kuwana akili timamu,.