Ali Kuachia Nyimbo Mbili na Kinywaji Cha Mo Faya Kuingia Sokoni
Staa wa muziki wa Bongo fleva nchini Ali Kiba ameweka wazi mipango yake ya kufungia mwaka 2018 ambapo ametangaza ujio wa nyimbo mbili na kinywaji chake cha Mo Faya kuingia sokoni.
Ali Kiba amesema ngoma hizo ataziachia kwenye shoo yake kubwa ya kufunga mwaka na muimbaji maarufu Afrika, Yvonne Chaka Chaka kutokea Afrika Kusini ikihairishwa hadi February, 2019.

BREAKING & EXCLUSIVE NEWS!!!! Kuelekea kwenye show yangu kubwa ya mwaka #FungaMwakaNaKingKiba tarehe 29 December pale @nextdoor_arena – nitaachia “HITS” zangu mbili kabla mwaka haujaisha pamoja na kuizindua rasmi kinywaji changu cha #MofayaEnergyDrink.
Sema kuna mabadiliko ya tarehe ya show yangu na Mama Yvonne Chaka Chaka pamoja na King Of Best Melodies @bellachristian – kutoka December to February 2019, the month of Love
:
Lakini sasa… siku hiyo ya tarehe 22 December 2018 si ndio FIESTA finale , so I’ll be performing katika Finale ya Msimu wa come back ya Fiesta na wanangu kutoka @kingsmusicrecords :
Na kumalizia mwaka basi tukutane Mombasa on New Year Eve tarehe 31 December —cheers to the New Year Mombasani!”.